Wednesday, July 5, 2017

Korea Kaskazini Yatoa Tishio na Maelezo kwa Kombora lao la Masafa marefu

Korea Kaskazini yatamba yasema Kombora lao linauwezo wa kufika Marekani

Korea Kaskazini ilitoa picha za kombora hilo la masafa marefu ICBM likirushwa

Marekani imethibitisha kwamba Korea kaskazini ilifanyia jaribio kombora la masafa marefu ambalo kulingana na wataalama wanaamini linaweza kufika Alaska Marekani.

Waziri wa maswala ya kigeni amelitaja jaribio hilo kuwa vitisho vipya kwa Marekani na dunia na kuonya kwamba Washington haitakubali hatua ya Korea Kaskazini kujihami na nyuklia.

Pyongyang imedai siku ya Jumanne kwamba ilifanikiwa kulifanyia majaribi kombora lake la masafa marefu ICBM.

Wakijibu, Marekani na Korea Kusini zilirusha makombora kusini mwa maji Korea.
Zoezi hilo la kijeshi la pamoja lililenga kuonyesha uwezo wa mashambulizi ya mataifa hayo mawili, Pentago imesema.

Ijapokuwa jaribio la Jumanne lilionekana kuwa hatua kubwa ,wataalam wanaamini kwamba Korea kaskazini haina kombora la masafa marefu la kinyuklia.

Bwana Tillerson pia alionya kwamba taifa lolote ambalo linasaidia kiuchumi na kijeshi Korea kaskazini ama limefeli kuidhinisha kwa ukamilifu maamuzi ya baraza la usalama ya Umoja wa Mataifa linasaidia utawala hatari.

Marekani imetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kujadili swala hilo.

Mkutano wa faragha wa wanachama wa baraza hilo unatarajiwa baadaye siku ya Jumatano.

Je Korea kaskazini ilisema nini siku ya Jumanne?

Tangazo hilo katika runinga ya taifa ya Korea kaskazini lilisema kuwa kombora hilo aina ya Hwasong -14 linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine lilisimamiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Ilisema kuwa kombora hilo liliruka umbali wa kilomita 2,802 na kusafiri kwa umbali wa kilomita 933 kwa dakika 39 kabla ya kuanguka baharini.

Korea Kaskazini imesema kuwa ni taifa lililojihami kinyuklia ambalo linamiliki kombora la masafa marefu linaloweza kushambulia eneno lolote duniani.

Marekani na Korea Kaskazini nini kimebadilika?

Chombo cha habari cha Korea kaskazini KCNA baadaye kilimnukuu Kim jong un akisema kuwa jaribio hilo ni zawadi kwa Wamerakani siku yao ya uhuru.

Jaribio hilo ambalo ni miongoni mwa majaribio ya makombora yake linakiuka marufuku ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Lakini wataalam wengi wanaamini kwamba Pyongyang bado haijakuwa na uwezo wa kutengeza kichwa cha kinyuklia kinachoweza kutosha katika kombora la masafa marefu na kwamba kombora kama hilo haliwezi kushambulia eneo linalolenga.

Je kombora hilo lina uwezo wa kusafiri umbali gani?

Swala kuu ni linaweza kusafiri kwa umbali gani, alisema mwandishi wa BBC Evans Seoul.
Je linaweza kushambulia Marekani?.

David Wright , kutoka muungano wa kisayansi anasema kuwa iwapo ripoti hiyo ni ya sawa ,kombora hilo linaweza kusafiri kwa umbali wa kilomita 6.700.

''Umbali huo unaweza kulifanya kufika Alaska, lakini sio visiwa vya Hawaii ama hata majimbo mengine 48 ya Marekani'',alisema.

''Sio kombora pekee ambalo Korea Kaskazini itahitaji'', mwandishi huyo anasema.

Pia ni lazime iwe na uwezo wa kulinda kichwa cha nyuklia kinapopaa angani na sio wazi iwapo Korea kaskazini ina uwezo huo.

Tuesday, July 4, 2017

HUYU NDIE AFISA WA POLISI ANAYEICHEZEA TIMU YA BLACK STARS GHANA

Afisa wa polisi anayeichezea Black Stars ya Ghana

Haki miliki ya pichaSAMUEL SARFOImage captionSamuel Sarfo kushoto ambaye alikuwa mlinzi sasa ni mchezaji mahiri wa Black Stars

Mwaka mmoja uliopita Samuel Sarfo afisa wa polisi nchini Ghana alipigwa picha , akiwalinda wachezaji wa timu ya soka ya taifa kabla ya mechi ya kimataifa.

Miezi 12 baadaye Sarfo mwenyewe ameichezea The Black Stars kwa mara ya kwanza akiingizwa kama mchezaji wa ziada katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Marekani katika mechi ya kirafiki iliochezwa mjini Connecticut siku ya Jumamosi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 pia ni nahodha wa klabu ya ligi ya taifa hilo Liberty Proffessionals na anachanganya uchezaji wake wa soka na kazi zake kama afisa wa polisi.

Mengi yamebadilika tangu aonekane na mavazi ya polisi , akilinda kikosi cha taifa na kama alivyomwambia mwandishi wa BBC Afrika Nishat Ladha ana mengi ya kumshukuru mwajiri wake.

Alisema kuwa anatimizi ndoto yake ya kuichezea timu ya taifa.

''Ni ndoto iliotimia.Hiyo ni ndoto ya kila kinda kuvaa jezi za timu ya taifa nchini Ghana''.

Amesema kuwa kiungo wa kati Emmanuel Agyemang-badu ambaye alipiga picha naye akivalia magwanda yake ya polisi na ambaye hakuchaguliwa katika timu hiyo dhidi ya Marekani amekuwa akimsadia sana.

Anasema kuwa anataka kucheza soka ya kulipwa kwa sababu ulimwengu unafaa kuona mchezo wake.

Source #BBCswahili

Monday, July 3, 2017

WATUHUMIWA WA ESCROW WAONGEZEWA MASHTAKA

Watuhumiwa wa kesi ya Escrow kuongezewa mashtaka nchini Tanzania

Saa moja iliyopita

Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpyaSambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Mshirikishe mwenzako

HakiGOOGLEImageMmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara James Rugemarila

Mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara James Rugemarila wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka 12, badala ya mashtaka sita waliyosomewa awali.

Miongoni mwa mashtaka hayo 12 ya uhujumu uchumi yamo mashtaka matano ya kutakatisha fedha na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27(USD 138,275.82).

Mashtaka hayo yanayowakabili ni pamoja na kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kuisababishia Serikali hasara na kutakatisha fedha.

Miongoni mwa mashtaka hayo ni kudaiwa, kati ya oktoba 18 ,2011 na Machi 19 , 2014 jijini Dar es Salaam ,Rugemarila na Sethi walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya Novemba 28/29, 2011 na Januari 23,2014 makao makuu Benki ya Stanbic kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi la St .Joseph kwa ulaghai washtakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), walijipatia USD 22,198,544.60 na Tsh 309, 461,300,158.27.

Vilevile Sethi ,anadaiwa kuwa kati ya Novemba 29, 2013 na Machi 14,2014 katika tawi la kati la Benki ya Stanbic Kinondoni Dar es Salaam alitakatisha fedha,Sh 309,461,300,158.27 kutoka BOT wakati akijua fedha hizo zimetokana na zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Januari 23,2014 katika benki ya Mkombozi tawi la St Joseph Cathedral, Rugemarila alitakatisha fedha USD 22,000,000 kutoka kwa Seth wakati akijua fedha hizo ni zao la uhalifu.

Hata hivyo,washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao.

Baaada ya kusomewa mashtaka hayo, wakili Shedrack Kimaro alidai upelelezi bado haujakamilika na washtakiwa wamepelekwa rumande hadi Julai14,217.

Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako